Sunday, February 2, 2014

LIFESTYLE : XCLUSIVELY TATTOOS ZA DRAKE NA MAANA YAKE

     Kwa jina kamili ni Aubrey Drake Graham ,akiwa kama ni msanii wa Hiphop na R&B kutoka kundi la YMCMB, Drake anaLifestyles tofauti za maisha yake ambapo mojawapo ni hii hapa ya kujichora tattoos ,blogu hii leo inakuletea Xclusively tattoos za Drake, ambazo amejichora kwenye mwili wake...

 Tazama Tattoo 10 za DRAKE HAPA CHINI...

  Hapo juu ni mgongo wa Drake ambao ni sehemu kubwa ya mwili wake ambayo ndio ina tattoos zake nyingi...sasa tuanze kuchambua moja baada ya nyingine...

 1.OVO OWL tattoo.

  Ukiangalia kwenye picha hapo juu,upande wa kulia chini kidogo ya bega lake la upande huo kuna tattoo ya Bundi ,hii tattoo inaitwa OVO OWL tattoo ambayo bundi huyo ni ishara ya Secret society iitwayo Bohemian Grove na imeambanishwa na maneno madogo yanayosema "If i die today, it'll be a holiday/atf/ovo/ymcmb/reps-up".


 2. AALIYA POTRAIT Tattoo.


   Ukiangalia kwenye Mgongo wake upande wa kushoto chin kidogo kuna tattoo ya aliyekuwa Msanii wa R&B, Aaliyah ambaye aliefariki mwaka 2001 kwa ajali ya ndege. Drake yuko obsessed na Aaliyah kwahiyo Dec.2011 aliamua kuchora tatto hii.

3. SONGBIRD tattoo.Juu  kidogo ya tattoo ya sura ya Aaliyah ,Drake anachora tattoo unayoiona hapo kushoto yenye maneno XO20 yenye wino mwekundu na mweusi. Maana ya hiyo number hapo ,20 ni crew ya marafiki zake ishirini.


4. Arm Tattoo of CN Tower.

Kama ilivokuwa kwa mzawa mwenzake ambaye ni Justin Bieber kutoka huko Toronto , Drake ni mtu wa kujisifu kwa huko alipotoka, hii CN TOWER, ni mnara wa mawasiliano ambao uko mjini jijini Toronto ambao ni kielelezo cha mji huo. Tattoo hii aliichora March, 2012.5. "ALL KINDS"Arm Tattoo.

February ,2012  Drake aliichora tattoo hii ndani kidogo ya mkono wake wa kulia.
6 . 416 Tattoo.

   Drake akiwa kama anafanya kazi zake za muziki U.S lakini hakutupi kwao na hii kama ilivokuwa tattoo zingine zizowakilisha mji wa kwao Toronto ,na hii inawakilisha Area code ya hiyo sehemu

 


7.  GRANDMOTHER & ANCLE Potrait Tattoo.

Kati ya  moja ya tattoo kubwa ni hii ambayo ipo nyuma ya mgongon mwake ambayo aliiyongeza mwilini mwake Dec,2012. Tattoo ni inaonesha mwanamke ambaye ni bibi yake mzaa mama,Evelyn Sher ambaye aliekuwa naye ni Pop star wa muziki kipindi hicho ,huku akimhug mjomba yake drake ambae pia nae alikuwa muimbaji . Drake anamkubali saana mjomba yake kwa mafanikio yake makubwa kwenye muziki na pia ukaribu wake kwa  mama mzaa mama yake,Sher.


8. MOTHER'S PORTRAIT Tattoo.

   Baada ya kuchora family portrait tattoo ya mjomba na Bibi yake, drake akaamua kumchora mtu kwenye mwili wake ambaye kwake ni muhimu sana si mwengine bali ni mama yake, Sandi Graham. Mama yake alimlea drake kwa kipindi chote baada ya kuachana na baba yake ambapo drake alikuwa na miaka mitano na sasa drake anasema mama yake ni mtu muhimu saana katika maisha yake.  

9.  HOUSTON STAR shoulder Tattoo.  

  November 18 ,2013, Drake aliamua kuongeza tattoo hii baada ya kuachia mshiko wa maana $17,000 katika strip club moja iitwayo Houston Strip club huko Texas.
10. FATHER'S PORTRAIT tattoo.


  Hivi karibuni January,2014 ,Drake aliamua kuchora tattoo ya sura ya baba yake mzazi, Denis Graham. Kwahiyo katika xperienca uliyoipata ndugu msomaji unaweza sasa kukubali kwamba Drake ni msanii ambaye anapenda saana Familia yake.

For MORE about drake in this site CLICK HERE..
Source : www.popstartats.com