R.I.P PAUL WALKER ( DEATH TRAGIC OF FAST & FURIOUS STAR PAUL WALKER)
(SANTA CLARITY CALIFORNIA)- PAUL WALKER star wa series ya sinema 'Fast & Furious' amefariki dunia Juma-mosi majira ya mchana akiwa na rafki yake katika ajali ya gari aina ya Porsche lenye rangi nyekundu, huko kaskazini ya Los Angels. Habari hiyo imetolewa na mwanajamii wake, Ame van Iden.
Katika Ukurasa wa Facebook ya Paul walker imeelezwa kuwa ,Paul walker alikuwa ni abiria katika gari hiyo ya rafiki yake, ambapo alikuwa katika eneo la kuhudhuria 'charity' ya 'organization' yake ya 'REACH OUT WORLDWIDE' .
Vyombo vya Dola huko Los Angels Vimeeleza kuwa ,walikuta gari Likiwaka moto Baaada ya kupata habari kuwa kuna ajali imetokea ambako watu wawili wamefariki dunia waliokuwa kwenye gari hiyo. Habari imeelezwa kuwa gari liligonga msitimu wa taa na kugonga mti na kulipuka kwa kuwaka moto.
Paul Walker amefariki dunia akiwa na miaka 40, na akiwa katika kazi yake ya muendelezo wa "Fast & Furious 7" ,na pia akiwa mmoja wa mastaa katika 'Drama' iitwayo 'HOURS'.
MUNGU AMREHEMU ...AMEIN!
Hizi ndio Picha za ajali ya PAUL WALKER
(angalia hapa chini)
Hii picha inaonesha usiku wa kuamkia leo ,Ma-fans wa PAUL WALKER wakiweka heshma ya Mishumaa na Maua katika mahali ambapo ajali ya kifo ilipotokea.