Tuesday, December 31, 2013

BIOGRAPHY : DAVIDO

Davido ,amezaliwa kama David Adedeji Adeleke ni mwmbaji wa muziki pia ni 'producer'. Davido ,akiwa kama mtoto wa Bw. na Bi. Adeleke alizaliwa Antlanta GA huko USA ,November 21st,1992, na kuhitimu 'British international school' huko lagos. na pia sasa anachukua degree yake ya Business administration kwa part time katika Babcock University.
Akiwa kama msanii ambaye anasafiri sana nchi kama USA ,UK  na Nigeria ,Davido ameXperience mila tofauti lakini hasahau kwao na hii ni inaaonesha hata katika muziki wake na watu ambao waliomuendeleza katika muziki kama Don jazzy ,2face idibia, Sound sultan, na wande coal.
Davido hata kama ameanza muziki hivi karibuni, lakini ameanza kuimba na kupafomu muziki tangu ana miaka 11 na mpaka sasa 21 na amezindua rekod Labo yake iitwayo HKN MUSIC, ambayo kwa pamoja inamilikiwa na Davido mwenyewe akiwa na kaka yake mkubwa Ade.
 Davido ,amejikusanyia mashabiki wengi katika kipindi cha muda mchache ambapo 2011 alizindua nyimbo yake ya kwanza akimshilikisha Naeto C ,iitwayo "Back When" , na baada ya Hapo akaja zaidi na kutoa singo ya Dami duro iliyotengenezwa na produza wake Shizzi na yeye pia ,Nov 2011 ambayo ilimpa wadhfa mkubwa katika tasnia ya muziki na kushika No#1 katika chati ya afrika ya Trace, na kujulikana zaidi nje ya afrika na Pia kupata nafasi kuimba katika jukwaa moja na wasanii wakubwa kama T-pain, Fabolous, Cabo snoop,Naeto C na wengine wengi.
Davido akiwa kama mwanamuziki na pia Balozi wa MTN ,anajulikana kama msanii ambaye yuko bize saana na muziki akiwa amefanya showz zikiwemo...
  • The Music Meets Runway Show
  • PSquare Invasion Concert
  • “This is Lynxxx” Campus Tour
  • Vivendi Fashion Show
  • Clan by Deola Sagoe
  • Loud on Sound Concert
  • Koko Concert London
  • Elite Model Look 2011 and many others
  • Rhythm Unplugged,
  • Echo 2011,
  • Access Bank End of year Party
  • The Sahara End of year concert.
 Na nyingine nyingi zikiendelea na kufanya tour nchi nyingi moja wapo nchi yetu ya Tanzania. Davido ni msanii mkubwa kwa sasa ambaye anatikisa tasnia ya muziki na ukweli huu unathibitishwa na Albamu yake ya kwanza iitwayo O.B.O(Omo Baba Olowo) iliyotoka mwaka 2011.

TAZAMA BAADHI YA PICHA ZA DAVIDO HAPA CHINI...

Akiwa na Familia Yake wa kwanza kushto ni kaka yake ambaye ni Chairman wa HKN music ,anaefatia ni baba yake Dr.Deji Adeleke, halafu dada yake Sharon

Huyu ni msanii mwenzake wa kundi la HKN MUSIC B-RED

Akiwa Na Akon
Akiwa na mchezaji mpira wa miguu Samuel Eto'o, huku wakionesha Rolex zaoo